Vivutio vya Kaskazini Mashariki mwa China vyenye hali ya hewa baridi vimekuwa vivutio vya “kidhahabu” kwa utalii wa majira ya joto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2024
Vivutio vya Kaskazini Mashariki mwa China vyenye hali ya hewa baridi vimekuwa vivutio vya “kidhahabu” kwa utalii wa majira ya joto
Picha iliyopigwa tarehe 8 Agosti 2024 inaonyesha hoteli ndani ya mbuga Ulan Maodu huko Hinggan, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Xinhua/Lian Zhen)

Vivutio vya utalii vya Kaskazini Mashariki mwa China, vilivyojulikana kwa mandhari yake ya theluji ya kipekee, baada ya kupata ukuaji wa shughuli za utalii msimu wa theluji mwaka jana, hivi sasa vinashuhudia hali ya kuongezeka kwa kiasi kikubwa watalii katika majira ya joto.

Eneo la Kaskazini Mashariki mwa China, ambalo linajivunia rasilimali zake nyingi za barafu na theluji, ambapo sehemu za misitu za eneo hilo ni kubwa zaidi, na wakati wa majira ya joto, hali ya hewa ya eneo hilo ni ya kufaa sana. Baada ya kujenga Sura ya aina mbili ya utalii, yaani utalii kwenye sehemu za barafu na theluji majira ya baridi, na utalii kwenye sehemu zenye hali ya hewa ya baridi kiasi cha kufaa majira ya joto, serikali za mitaa za eneo hilo zimeanzisha njia ya maendeleo ya kwenda sambamba kwa ulinzi wa ikolojia na ukuaji wa uchumi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha